Home / Sécurité / UJUMBE WA POLE NA MSIMAMO MKALI KWA WANAICHI WA FIZI

UJUMBE WA POLE NA MSIMAMO MKALI KWA WANAICHI WA FIZI

Wananchi wa Wilaya ya Fizi,
Ndugu zangu,

Ninazungumza nanyi kwa maumivu makubwa na hasira ya haki kwa sababu ya mateso makubwa mnayopitia. Vita vinavyoendelea Fizi na Mashariki ya Kongo si bahati mbaya. Ni matokeo ya kutokujali, uzembe na kuachwa kwa wananchi.

Natoa pole zangu za dhati kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao. Ninasimama pamoja na wanawake, watoto na wazee ambao wamelazimika kukimbia makazi yao na leo wanaishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao au katika inchi jirani. Hii hali ni aibu kubwa.

Wanainchi wa Fizi, bila kujali kabila, lugha au dini—Babembe, Bafuliru, Banyamulenge na jamii zote za eneo letu—sisi ni watu wamoja, mateso yetu ni moja, na hatima yetu ni moja. Tusikubali kugawanywa. Kuna ndugu anaweza kutuhelezea kwa nini Wa généraux wetu Sikatenda na Aoci wamefungwa mpaka kupoteza maisha gerezani na mpaka leo awajazikwa, ni kwa nini? Kwa nini Général Mutupeke na Colonel Antoine wako nazimika polepole gerezani mpaka leo?

Haikubaliki kwamba leo, raia wa Kongo wanateseka huku Serikali ikishindwa kuwalinda. Wanainchi wa Fizi hawawezi kuendelea kuachwa peke yao. Hii hali lazima ibadilike.

Kama mwana wa Fizi na Mbunge wa Heshima, ninakemea vikali hali hii na ninadai:

ulinzi wa haraka kwa raia; na kufunguliwa kwa maoffisa wetu;

msaada wa dharura kwa wakimbizi;

ukweli juu ya vita hivi;

na amani ya kudumu, si maneno matupu.

Kwa jumuiya ya kimataifa nasema: maneno hayatoshi. Mateso ya watu wa Fizi hayawezi kuendelea bila hatua.

Kwa wanainchi wa Fizi: maumivu yenu yanaeleweka, hasira yenu ni ya haki. Msikate tamaa. Simameni imara pamoja.

Amani itarudi, lakini kwa haki na ukweli, si kwa kusahau mateso yenu.

Imeandikwa kwa maumivu na hasira moyoni,

Profesa Nehemia Mwilanya
Mbunge wa Heshima wa Wilaya ya Fizi

Répondre

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *