Tokea kuanzisha kazi za Matunzo mjini Bukavu clinique de l’Oeil de Bukavu imekuja kuwa saidiya raiya wengi hasa wale wanao gonjwa macho, kulingana na Mazungumzo pamoja mganga Mkuu kwenye kituo hicho yeye na wapasha habari wa OeilTaifa Africa, Dr Matthias ameonyesha kuwa tayari kazi zaku pasua wagonjwa mecho (Chirurgie) zimeanza na nikwa bei raïsi katika lengo la kuwasaidiya raia wa Bukavu na kandokando yake.

Duru letu huonyesha kuwa wagonjwa vipofu ambao tayari sasa ni miaka 2,4,10,14 wamefungwa macho wameanza ona kupitiya ma Daktari wa clinique hiyo, na ndio maana ameomba raia wa Bukavu ambao wamekuwa na shida ya macho kupita kwenye clinique de l’Oeil de Bukavu ili wajipimishe maana hadi sasa vipimo ni bure. kama alivyo akikisha Dr Matthias

Kumbukeni kuwa clinique de l’oeil de Bukavu yapatikana mtaani ibanda kifuani na SONAS njiaa inayo enda kwenye ofisi la DGI Mjini Bukavu
Régine MUPENDA








